Tuesday, September 20, 2016

TANESCO KIGAMBONI MALIZA TATIZO LA KUKATIKA UMEME - DC Mgandilwa

Leo tarehe 20/9/2016 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh Hashim Mgandilwa amefanya ziara katika Ofisi za TANESCO wilaya ya Kigamboni.

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh Hashim Mgandilwa akizungumza na wafanyakazi TANESCO

Baada ya kutembelea Ofisi mbalimbali na kujionea hali halisi ya utendaji kazi alizungumza na uongozi na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

DC Mgandilwa pamoja na kuwapongeza wafanyakazi kwa juhudi zao za kila siku kuboresha huduma za upatikanaji wa umeme wilayani hapa, alikemea vikali mambo ambayo yanasababisha kuzorota kwa huduma hiyo mara kadhaa. 

Amewataka kuboresha mifumo ya umeme na kumaliza tatizo la kukatikakatika kwa umeme kila mara. Pia amesisitiza utoaji wa taarifa kwa wananchi kabla ya kukata umeme pale inapowalazimu kufanya hivyo kwa sababu za msingi.

Amewakumbusha wafanyakazi hao dhana ya uwajibikaji katika nafasi walizonazo ili kuwaletea wananchi maendeleo na kuwa yeye hatasita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atalayeleta uzembe na tabia zisizokubalika zenye kusababisha huduma mbovu kwa wananchi. 

DC Mgandilwa aliwataka viongozi wa taasisi hiyo kutengeneza ushirikiano mzuri na viongozi wa ngazi mbalimbali ili kurahisisha kuwafikia na kuwahudumia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa. 

Pia Mkuu wa wilaya amewataka TANESCO kuharakisha taratibu za ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilaya ya Kigamboni zinazotarajiwa kujengwa eneo la Somangila na kusisitiza matumizi mazuri na sahihi ya pesa itakayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hizo. 
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO mkoa wa Temeke Eng. Jahulula M. Jahulula aliyeko kulia, kushoto ni Meneja wa TANESCO wilaya ya Kigamboni Eng. Richard S. Widimael 



Katibu tawala wa wilaya ya Kigamboni Ndg Cosmas Hinju akizungumza katika kikao hicho





Sehemu ya wafanyakazi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya

Sunday, September 18, 2016

SASA KIGAMBONI KUONGEZA UFAULU FORM IV KWA MWENDO KASI

Kikao cha wadau wa elimu Kigamboni chatoa majibu....

DC Mgandilwa asema ufaulu lazima uongezeke....


Wazazi wasio wafatilia maendeleo ya watoto wao shule na kuwaozesha kuishia jela...


Tarehe 17/9/2016 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa alikutana na wadau wa Elimu Kigamboni kujadili changamoto za elimu na kupendekeza namna ya kuzitatua. 

Waliohudhuria ni pamoja na wadau wa elimu Kigamboni, wanafunzi wa vyuo,  Wahitimu wa Vyuo, na wadau wa maendeleo waliopo ndani na nje ya wilaya ya Kigamboni. 

Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Mgandilwa kutoa hali halisi ya hali ya elimu wilayani humo, kabla ya kuwakaribisha wadau kwa michango na maoni yao alikemea baadhi ya mambo ambayo yanafanywa na wazazi yanayorudisha nyuma maendeleo ya kitaaluma kwa watoto wao. 

"......kuanzia sasa mzazi atakayeshiriki kumuachisha shule na kumuozesha mtoto wake atachukuliwa hatua kali za kisheria....., watoto wote lazima tuhakikishe wanasoma na kumaliza..... " Alisema DC Mgandilwa. 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa akizungumza na wadau wa Elimu, Kulia ni Mama Mpangala Kaimu Afisa Elimu ya Sekondari Wilayani humo

Pia aliongeza kuwa manispaa ya Kigamboni iko mbioni kutengeneza Sheria ndogondogo zitakazowabana wazazi kufatilia mienendo na maendeleo ya watoto wao mashuleni.

".....haiwezekani serikali inachukua hatua za makusudi za kuwapa elimu bure, kuwapa madawati ya kutosha, kujenga vyumba vya madarasa na mahabara alafu wewe mzazi ushindwe kufatilia mtoto wako kama anafika shule au unaishia beach na kwenye makundi ya kihuni akifeli unaanza kulaumu serikali...." alionya DC Mgandilwa. 

Baadae Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa wadau waliohudhuria kuchangia kwa Uhuru na kupendekeza namna gani ya kuboresha elimu Kigamboni. DC Mgandilwa alisema Ofisi yake ingeweza kufanya maamuzi lakini amewashirikisha wadau ili waone hili ni jambo lao wenyewe, washirikiane katika kuboresha elimu. 

Baada ya maoni na michango mbalimbali kikao hicho chini ya Mkuu wa Wilaya kilifikia maazimio. Maazimio ya Muda mfupi ni pamoja na:-

i). Kuanzisha mfuko wa elimu Kigamboni ambao utasaidia kutatua dharula za kielimu kwa wakati pindi zinapotokea kuliko kusubiri na kuomba pesa serikalini.

ii) Kuimarisha idara ya ukaguzi wa shule ili kuwafanya wahusika kuwajibika zaidi na kufanya shule zitekeleze adhima iliyokusudiwa kwa ufanisi.

iii) Kuanzisha mitihani ya ujirani mwema ili kuongeza ushindani miongoni mwa wanafunzi. 

iv) Kuanzisha Solving Special Program. Hii italenga kuwafanya wahitimu na wanavyuo kujitolea kufanya solving ya maswali mbalimbali na kuwapa mbinu za kujibu mitihani wanafunzi hasa kwa kuanzia na walio kidato cha nne sasa hivi ili kupunguza Failures. 
Hii itajikita zaidi katika masomo ya sayansi na biashara. 

Maazimio ya Mipango ya muda mrefu ni:-

i) Kutumia Walimu wa sayansi watakaokuwepo kufundisha shule zaidi ya moja ili kuziba upungufu kwa shule zisizo na Walimu hao kabisa. 

ii) Kufanya mitihani ya kila wiki ili kuwajengea wanafunzi tabia za kujisomea kila mara. 

iii) DC kukamilisha mpango wake wa kutengeneza forum ya wasomi Kigamboni wenye taaluma mbalimbali watakaosaidia kuboresha sekta ya elimu. 

iv) Maandalizi ya kutengeneza Makataba ya Mtandaoni (E-library) itakayosaidia wanafunzi kupata vitabu vyote kwenye mtandao na kujisomea ndani ya maktaba hiyo. Hii itaendana na ukuaji wa sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) 

v)  Ujenzi wa mabweni ya wanafunzi kwenye shule zenye uhitaji huo ili wanafunzi wakae shuleni na kupata muda wa kutosha kujisomea. 

Kwa mujibu wa tamko la DC Mgandilwa Maazimio ya Muda mfupi yaliyofikiwa yataanza kutekelezwa mara moja. 

Aidha, wadau wa elimu, maendeleo ya Kigamboni na yeyote anayeguswa ambaye hakuweza kufika kikaoni hapo DC Mgandilwa alisema kuwa asisite kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni kupeleka maoni yake au kupeleka taarifa zake ili ashirikishwe kwenye Forum ya wasomi Kigamboni. Pia anaweza kutuma maoni na taarifa zake kwenda 0719828676 zitapokelewa na kufanyiwa kazi.wa




Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Cosmas Hinju akizungumza na wadau wa Elimu



Wadau wakiwa kikaoni



Wadau wakiwa kikaoni

 Wadau wakiwa kikaoni


Wednesday, September 14, 2016

Leo asubuhi majira ya saa mbili hadi saa tatu asubuhi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.  Hashim Mgandilwa alikuwa live ndani ya 93.7Efm Radio.


Amezungumzia mambo mbalimbali ya Kigamboni lakini kubwa zaidi ni kampeni anayotaka kuifanya ya kuinua ufaulu wa wanafunzi wa Kigamboni na fursa zilizopo kwa ajili ya vijana wasomi ili kufanikisha program hiyo. 

"....wewe kama mdau wa elimu, mdau wa maendeleo au kijana msomi uliopo chuo na muhitimu wa chuo ulie Kigamboni au nje, karibu tuzungumze namna ya kupandisha ufaulu wa wanafunzi wetu. Tukutane tarehe 17/9/2016 saa 4:00asubuhi katika chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere..." Alisema DC Mgandilwa  

Thibitisha kushiriki sasa kupitia namba 0719828676 

Kigamboni ni yetu sote,
Tushirikiane kupandisha ufaulu wa wanafunzi wetu.

Tuesday, September 13, 2016

PAMOJA TUPANDISHE UFAULU WA WANAFUNZI KIGAMBONI

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa anatarajia kuwa na Kikao cha Wadau wa Elimu katika wilaya ya Kigamboni siku ya Jumamosi tar 17/09/2016 Saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Chuo cha Mwl Nyerere.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa 

Lengo la kikao hicho ni kutafuta namna ya Kukabiliana na Changamoto za Elimu hususani Kupandisha Ufaulu wa Wanafunzi wetu wa Shule za Sekondari ndani ya Wilaya yetu Mpya.

Walengwa wa kikao hiki ni Wadau wa Elimu, Wadau wa Maendeleo Kigamboni, Wanavyuo, Wahitimu wa Vyuo wanaotokea Kigamboni, Viongozi wote wanaoguswa na Wapenda Maendeleo ya Kigamboni waishio ndani na nje ya Wilaya yetu.

Hivyo wewe kama Mdau muhimu kwa Maendeleo ya Sekta ya Elimu Kigamboni unakaribishwa sana, Tafadhali thibitisha Ushiriki wako kwa Kutuma Jina lako kamili na Namba yako ya Simu kwenda 0719828676, Mwisho ni tar 15/09/2016.

#Kigamboni ni yetu sote,
#Tushirikiane kupandisha Ufaulu wa Wanafunzi wetu.

Tafadhali Mjulishe na mwenzako...

Imetolewa na,
Hashim Mgandilwa
DC Kigamboni

Thursday, September 8, 2016

NAHITAJI BARUTI ZA KUULIA SAMAKI-DC Mgandilwa

SOKO LA SAMAKI LA KISASA LINAKUJA - Mkurugenzi Katemba. 

Tarehe 7/9/2016 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa aliyeambatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba wamewatembelea wavuvi  wanaofanya shughuli zao maeneo ya Feri.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe.  Hashim Mgandilwa akisisitiza jambo wakati anazungumza na wavuvi, aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba 

#DC Mgandilwa akemea vikali uvuvi haramu unaombatana na kuvua kwa kutumia mabomu na baruti.

#Aagiza Polisi kusaka baruti mahali popote zilipo na kumfikishia, anuia kutokomeza uvuvi haramu Kigamboni.

#Pia amewaonya wote wanaochafua mazingira ya ufukwe wa bahari kuacha mara moja.

# Atakayekamatwa akichafua mazingira ya ufukwe wa bahari kutozwa faini Sh 50,000/- na Sh 20,000/- kupewa atakayemkamata.

#Mkurugenzi Katemba awahakikishia wavuvi kujenga soko la Samaki la kisasa.

#Soko hilo kuwa chanzo cha mapato ya Manispaa ya Kigamboni.

#Awataka wafanya biashara wanaostahili kulipa kodi kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria kwani kodi zitasaidia Serikali kuboresha huduma za jamii na miundombinu.

#Asema hakuna mnyonge atakayeonewa, wafanya biashara ndogondogo hawatalipishwa kodi zisizo za lazima.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba









Wednesday, September 7, 2016

WADAU KARIBU KIGAMBONI TUZUNGUMZE - DC Mgandilwa

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa anatarajia kuwa na Kikao cha Wadau wa Elimu katika wilaya ya Kigamboni siku ya Jumamosi tar 17/09/2016 Saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Chuo cha Mwl Nyerere.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa 

Lengo la kikao hicho ni kutafuta namna ya Kukabiliana na Changamoto za Elimu hususani Kupandisha Ufaulu wa Wanafunzi wetu wa Shule za Sekondari ndani ya Wilaya yetu Mpya.

Walengwa wa kikao hiki ni Wadau wa Elimu, Wadau wa Maendeleo Kigamboni, Wanavyuo, Wahitimu wa Vyuo wanaotokea Kigamboni, Viongozi wote wanaoguswa na Wapenda Maendeleo ya Kigamboni waishio ndani na nje ya Wilaya yetu.

Hivyo wewe kama Mdau muhimu kwa Maendeleo ya Sekta ya Elimu Kigamboni unakaribishwa sana, Tafadhali thibitisha Ushiriki wako kwa Kutuma Jina lako kamili na Namba yako ya Simu kwenda 0719828676, Mwisho ni tar 15/09/2016.

#Kigamboni ni yetu sote,
#Tushirikiane kupandisha Ufaulu wa Wanafunzi wetu.

Tafadhali Mjulishe na mwenzako...

Imetolewa na,
Hashim Mgandilwa
DC Kigamboni

WACHINA WAITAMANI KIGAMBONI


_❗Wanuia Kufanya Uwekezaji Mkubwa....._

_❗Kigamboni kutoa ajira nyingi sana...._

Tarehe 30/8/2016 Viongozi wa Wilaya ya Kigamboni wakiongozwa na Mkuu wa *Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba* walikutana na kufanya mazungumzo na *Ujumbe wa Wawekezaji* kutoka katika *Jimbo la Sichuan nchini China.*


Katika mazungumzo hayo, *Uongozi wa Wilaya ya Kigamboni uliwakaribisha wawekezaji hao kuwekeza zaidi katika maeneo yafuatayo:-*

*1. Kujenga Kituo kikubwa cha masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano -TEHAMA (ICT Hub)*

*2. Uvuvi na kuongeza thamani kwenye mazao ya bahari*

*3. Viwanda vya Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.*

*4. Huduma za jamii: Ujenzi wa Hospitali na Majengo Makubwa ya biashara (Shopping Malls).*

Kwa upande wao ujumbe wa *Wawekezaji kutoka China* ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kongresi ya watu wa Sichuan Ndugu Zhang Dong Sheng ulikubaliana na vipaumbele walivyopewa kuwekeza huku wakisisitiza nia yao ya dhati kurudi hivi karibuni kwa ajili ya hatua za Uwekezaji zinazofuata. Jimbo la Sichuan ni la sita kwa kiuchumi katika nchi ya China.

*#KigamboniYetu,FahariYetu.*