Wednesday, September 7, 2016

WADAU KARIBU KIGAMBONI TUZUNGUMZE - DC Mgandilwa

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa anatarajia kuwa na Kikao cha Wadau wa Elimu katika wilaya ya Kigamboni siku ya Jumamosi tar 17/09/2016 Saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Chuo cha Mwl Nyerere.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa 

Lengo la kikao hicho ni kutafuta namna ya Kukabiliana na Changamoto za Elimu hususani Kupandisha Ufaulu wa Wanafunzi wetu wa Shule za Sekondari ndani ya Wilaya yetu Mpya.

Walengwa wa kikao hiki ni Wadau wa Elimu, Wadau wa Maendeleo Kigamboni, Wanavyuo, Wahitimu wa Vyuo wanaotokea Kigamboni, Viongozi wote wanaoguswa na Wapenda Maendeleo ya Kigamboni waishio ndani na nje ya Wilaya yetu.

Hivyo wewe kama Mdau muhimu kwa Maendeleo ya Sekta ya Elimu Kigamboni unakaribishwa sana, Tafadhali thibitisha Ushiriki wako kwa Kutuma Jina lako kamili na Namba yako ya Simu kwenda 0719828676, Mwisho ni tar 15/09/2016.

#Kigamboni ni yetu sote,
#Tushirikiane kupandisha Ufaulu wa Wanafunzi wetu.

Tafadhali Mjulishe na mwenzako...

Imetolewa na,
Hashim Mgandilwa
DC Kigamboni

WACHINA WAITAMANI KIGAMBONI


_❗Wanuia Kufanya Uwekezaji Mkubwa....._

_❗Kigamboni kutoa ajira nyingi sana...._

Tarehe 30/8/2016 Viongozi wa Wilaya ya Kigamboni wakiongozwa na Mkuu wa *Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba* walikutana na kufanya mazungumzo na *Ujumbe wa Wawekezaji* kutoka katika *Jimbo la Sichuan nchini China.*


Katika mazungumzo hayo, *Uongozi wa Wilaya ya Kigamboni uliwakaribisha wawekezaji hao kuwekeza zaidi katika maeneo yafuatayo:-*

*1. Kujenga Kituo kikubwa cha masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano -TEHAMA (ICT Hub)*

*2. Uvuvi na kuongeza thamani kwenye mazao ya bahari*

*3. Viwanda vya Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.*

*4. Huduma za jamii: Ujenzi wa Hospitali na Majengo Makubwa ya biashara (Shopping Malls).*

Kwa upande wao ujumbe wa *Wawekezaji kutoka China* ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kongresi ya watu wa Sichuan Ndugu Zhang Dong Sheng ulikubaliana na vipaumbele walivyopewa kuwekeza huku wakisisitiza nia yao ya dhati kurudi hivi karibuni kwa ajili ya hatua za Uwekezaji zinazofuata. Jimbo la Sichuan ni la sita kwa kiuchumi katika nchi ya China.

*#KigamboniYetu,FahariYetu.*