Tarehe 7/9/2016 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa aliyeambatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba wamewatembelea wavuvi wanaofanya shughuli zao maeneo ya Feri.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa akisisitiza jambo wakati anazungumza na wavuvi, aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba
#DC Mgandilwa akemea vikali uvuvi haramu unaombatana na kuvua kwa kutumia mabomu na baruti.
#Aagiza Polisi kusaka baruti mahali popote zilipo na kumfikishia, anuia kutokomeza uvuvi haramu Kigamboni.
#Pia amewaonya wote wanaochafua mazingira ya ufukwe wa bahari kuacha mara moja.
# Atakayekamatwa akichafua mazingira ya ufukwe wa bahari kutozwa faini Sh 50,000/- na Sh 20,000/- kupewa atakayemkamata.
#Mkurugenzi Katemba awahakikishia wavuvi kujenga soko la Samaki la kisasa.
#Soko hilo kuwa chanzo cha mapato ya Manispaa ya Kigamboni.
#Awataka wafanya biashara wanaostahili kulipa kodi kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria kwani kodi zitasaidia Serikali kuboresha huduma za jamii na miundombinu.
#Asema hakuna mnyonge atakayeonewa, wafanya biashara ndogondogo hawatalipishwa kodi zisizo za lazima.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba