Friday, July 8, 2016

MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI AAPISHWA

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakuu wapya wa wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi kwa kujituma katika kuwatumikia wananchi na atakayeshindwa atamshauri Rais amtafutie wilaya nyingine.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutubia wananchi katika hafla ya  kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam Julai 4, 2016.
Amesema kuwa wakuu wa wilaya wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni kupiga marufuku uvutaji wa shisha katika mkoa wa Dar es Salaam, Uvutaji Sigara hadharani na wataofanya hivyo watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Makonda amesema kuwa operesheni ya kuondoa ombaomba bodo inaendelea na wakuu wilaya wametakiwa kusimamia operesheni hiyo kutokana na mazingira mazuri ya elimu yaliyowekwa kwa watoto hao kusoma ili waweze kuachana na utegemezi huo.

Makonda amesema kuwa watu wanaowasaidia wanaomba wanafanya makosa kwa kufanya watu hao washindwe kuondoka katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa tatizo la madawati bado lakini kuna upungufu wa vyumba vya madawati ambayo ni muhimu katika kuweza kuainisha katika kipindi hiki.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam  Julai 4, 2016.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam  Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam Julai 4, 2016.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akijibu maswali ya Waandishi wa habari namna alivyojipanga kuwatumikia wanaKigamboni mara baada ya kuapishwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam Julai 4, 2016.


Wakuu wa Wilaya kama walivyokaa kutokea kushoto Sophia Mjema - Ilala, Hashim Mgandilwa - Kigamboni, Salum Hapi - Kinondoni na Felix Lyaviva - Temeke wakijiandaa kula kiapo.

 
Sehemu ya wananchi waliohudhuria kuapishwa kwa Wakuu wa Wilaya

 Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Wakuu wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam mara baada ya kuapa, nyuma yao ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es salaam