MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakuu wapya wa
wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi kwa kujituma katika
kuwatumikia wananchi na atakayeshindwa atamshauri Rais amtafutie wilaya
nyingine.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutubia wananchi katika hafla
ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam
Julai 4, 2016.
Amesema
kuwa wakuu wa wilaya wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni kupiga
marufuku uvutaji wa shisha katika mkoa wa Dar es Salaam, Uvutaji Sigara
hadharani na wataofanya hivyo watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Makonda
amesema kuwa operesheni ya kuondoa ombaomba bodo inaendelea na wakuu
wilaya wametakiwa kusimamia operesheni hiyo kutokana na mazingira mazuri
ya elimu yaliyowekwa kwa watoto hao kusoma ili waweze kuachana na utegemezi huo.
Makonda
amesema kuwa watu wanaowasaidia wanaomba wanafanya makosa kwa kufanya
watu hao washindwe kuondoka katika jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida, wakati alipowasili kwenye
ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya
wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya
Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
salaam Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na
Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa mara baada
ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam Julai
4, 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akijibu maswali ya Waandishi wa habari namna alivyojipanga kuwatumikia wanaKigamboni mara baada
ya kuapishwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam Julai
4, 2016.
Wakuu wa Wilaya kama walivyokaa kutokea kushoto Sophia Mjema - Ilala, Hashim Mgandilwa - Kigamboni, Salum Hapi - Kinondoni na Felix Lyaviva - Temeke wakijiandaa kula kiapo.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria kuapishwa kwa Wakuu wa Wilaya
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Wakuu wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam mara baada ya kuapa, nyuma yao ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es salaam
safi
ReplyDeleteKARIBU Z4NEWSBLOG.BLOGSPORT.COM
ReplyDelete