❗Waliovamia maeneo ya Shule, Zahanati na wasioendeleza maeneo yao kukiona....
❗Watakao tumia vibaya pesa za Elimu bure na Afya kuishia gerezani....
❗Aweka jiwe la msingi majengo Mapya ya Hospitali iliyoanzishwa Kigamboni na Baba wa Taifa 1961....
Leo tarehe 27/8/2016 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Steven Katemba ameshiriki zoezi la kufanya usafi kama ulivyo utaratibu wa Manispaa hiyo kufanya Usafi kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi.
Ameanza usafi saa 12:00 asubuhi katika Hospitali ya Mji Mwema kabla ya kuungana na DC wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa aliyekuwa akishirikiana na wananchi kufanya Usafi katika eneo la Tungi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni pamoja na mambo mengine, aliweka Jiwe la Msingi katika majengo mapya ya Hospitali ya Mji Mwema yanayojengwa kwa msaada wa taasisi ya MDH. Hospitali hiyo ilianzishwa tarehe 14 January 1961 na Jengo lake la kwanza liliwekwa Jiwe la Msingi na Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius K. Nyerere aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika kipindi hicho.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni wakati alipoweka jiwe la msingi
Akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi, Ndg Katemba amesema haridhishwi na usafi wa mazingira tu unaofanyika kila mwisho wa mwezi bali usafi wa mazingira uendane na Usafi wa Nafsi.
".....nataka usafi wa mazingira tunaoufanya uendane na usafi wa nafsi zetu, haiwezekani leo tumefanya usafi wa mazingira ya Hospitali yamependeza lakini watu wakija wapate huduma mbovu......." Alisema Katemba
Ameongeza kuwa watumishi wanatakiwa kubadilisha fikra zao na kuwahudumia wananchi kwa Upendo na kwa Kuzingatia Weledi na Maadili ya kazi yao.
Pia amewataka wananchi kushirikiana vyema na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni akisisitiza Usafi wa Nafsi kwa Watumishi kuwa ni kufanya kazi ya kutatua matatizo ya wananchi na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Amewatahadharisha watu wote Waliovamia maeneo ya Shule na Zahanati kurudisha maeneo hayo haraka kabla hawajafuatwa.
Pia amewataka wote ambao walichukua maeneo makubwa kwa ajili ya kuyaendeleza kufanya hivyo mara moja kabla hawajanyang'anywa.
Mkurugenzi Katemba amewataka wananchi kuendelea kujituma kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo kwani zama hizi ni za Kazi tu! na wasitegemee maneno mazuri muda wote wa kazi.
"......unapokuja ofisini usitegemee maneno matamu Sana, mimi nimekuja kufanya kazi...., mtu kama kavamia eneo la serikali au Shule au Zahanati unapoenda kubomoa huwezi kwenda unacheka kwa maneno matamu....., Wakati wa kazi iwe Kazi tu....!"
Aidha, Mkurugenzi Katemba katika kuunga mkono juhudi za wananchi na wahisani wanaojenga majengo mapya ya Hospitali kwa ajili ya Vitengo vya Kifua Kikuu na VVU/Ukimwi ametoa mchango wa mifuko 20 ya Sementi itumike katika ujenzi huo.
Awali, akiwasilisha changamoto za Hospitali hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mji Mwema Ndg Omary Kombe alimuomba mkurugenzi kusaidia ulipaji wa fidia za maeneo ya pembeni ya Hospitali ili iweze kupanuliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh Hashim Mgandilwa katika zoezi la usafi
Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni atika zoezi la usafi